Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Djibouti yaelimishwa kuhusu athari za uhamiaji:IOM

Djibouti yaelimishwa kuhusu athari za uhamiaji:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ofisi ya Nairobi Kenya limekuwa likifanya warsha ya ulelimishaji nchini Djibouti kuifahamisha serikali kuhusu uingiaji wa wahamiaji.

IOM katika warsha hiyo linazungumzia uingiaji wa mchanganyiko wa wahamiaji, hatari za hatua hiyo, athari kwa wahamiaji na jamii zinazowapokea nchini Djibouti na hatua zinazochukuliwa na IOM kukabiliana na changamoto hizo. Warsha hiyo pia imeanzisha suala za haki za wahamiaji katika misingi ya sheria za kimataifa na za Kiislam. Djibouti ina changamoto tofauti za wahamiaji hasa kutokana na eneo hilo kuwa njia panda ya Ulaya, Asia na Afrika.

Pia ni kituo cha kuondokea watu wengi kutoka pembe ya Afrika kwenda Mashariki ya Kati na pia kwenye maeneo ya Ghuba ya aden na kwingineko. Kila mwaka maelfu ya wahamiaji wa Eritrea, Ethiopia na Somalia wanaingia Djibouti wakikimbia vita, njaa na umasikini katika nchi zao.