Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeomba ifadhiliwe misaada ya kunusuru maisha ya wahamiaji wa Usomali wanaokabiliwa na mafuriko Kenya

UNHCR imeomba ifadhiliwe misaada ya kunusuru maisha ya wahamiaji wa Usomali wanaokabiliwa na mafuriko Kenya

Shirika la UNHCR limetoa ombi maalumu linalowataka wahisani wa kimataifa kuchangisha msaada wa dharura wa dola milioni 2.8 zinazohitajika kushughulikia hatari ya mafuriko, inayowakabili watu 300,000,

wingi wao wakiwa wahamiaji Wasomali wanaoishi kwenye makazi ya muda ya kambi za Kakuma, ziliopo katika kaskazini-magharibi, nchini Kenya na kwenye kambi ya mashariki ya Dadaab, karibu na mipaka na Usomali. Kwa mujibu wa ripoti, maeneo haya hukabiliwa na matatizo ya mafuriko, takriban kwa miezi mitatu, kila mwaka. Ripoti inasema mvua zilipoanza kunyesha kwenye eneo hilo, wiki tatu zilizopita, UNHCR ililazimika kuchimba mitaro na mahandaki, na kuzingia majengo ya hospitali, na kwenye visima, na sehemu nyengine muhimu, magunia ya michanga ili kuyakinga na mafuriko.