UM umeingiwa wasiwasi juu ya kuzuka mapigano ya kikabila katika JKK kuhusu haki ya uvuvi

UM umeingiwa wasiwasi juu ya kuzuka mapigano ya kikabila katika JKK kuhusu haki ya uvuvi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuingiwa wasiwasi mkubwa juu ya mapigano makali ya kikabila yalizuka wiki iliopita, kwenye jimbo la Equateur, katika JKK, juu ya haki za uvuvi.

Imeripotiwa watu 60 waliuawa na watu 40 walijeruhiwa, hali ambayo ilisababisha wakazi 16,000 kung'olewa makazi na kukimbilia kwenye maeneo jirani ya JKK. Vile vile UNHCR imeripoti vijiji kadha vilichomwa mooto, hali ambayo imeilazimisha UM kutuma timu ya uchunguzi kwenye eneo, kuchanganua mahitaji hakika ya kiutu ya umma waathirika, ambao wanahitajia makazi ya muda ya kujistiri na huhitajia chakula, halkadhalika, pamoja na vifaa vya nyumbani - mathalan, mablanketi, vitu vya jikoni na majerikeni.