Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO inatabiri kukithiri kwa wasiyekuwa na kazi duniani katika 2009

ILO inatabiri kukithiri kwa wasiyekuwa na kazi duniani katika 2009

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) amewasilisha ripoti mpya, kwa kupitia Geneva, yenye kutabiri idadi ya watu wasiyekuwa na kazi mwaka huu, itaongezeka kwa kima cha baina ya watu milioni 39 hadi milioni 59.

Alisema mkutano wa mwaka wa ILO, utakaofanyika Geneva kuanzia tarehe 3 mpaka 19 Juni (2009), utazingatia namna ya kufikia "maafikiano ya kuzalisha ajira" ya dharura ulimwenguni, kwa lengo la kuendeleza sera ya pamoja, itakayosaidia umma wa kimataifa kukabiliana vyema na matatizo ya ukosefu wa kazi katika dunia.