Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa UNRWA athibitisha huduma za afya zimefufuliwa Ghaza kufuatia mapigano

Mkurugenzi wa UNRWA athibitisha huduma za afya zimefufuliwa Ghaza kufuatia mapigano

Dktr Guido Sabatinelli, Mkurugenzi wa Afya wa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kiutu kwa Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA), kwenye mazungumzo na waandishi habari mjini Geneva alielezea juu ya hali dhaifu iliokabili sekta ya afya, ambayo imeharibika zaidi kutokana na mashambulio ya wiki tatu zilizopita.

"Kama mnavyoelewa, UNRWA inahudumia watu 750,000 tuna mtandao wa zahanati mbalimbali, na pindi hatuwezi kuwapatia matibabu watu muhitaji, huwapeleka kwenye mahospitali wale wenye kuhitajia uangalizi ziada. Mwelekeo tulionao sasa hivi ni kuhakikisha tunafufua haraka zile huduma zote za afya zinazoendeshwa na UNRWA. Hii leo tuna ripoti nzuri, na za kutia moyo, kwamba vituo 17 vya afya vya UNRWA, vimeshaanza kufanya kazi, na asilimia 60 ya wahudumia afya wamesharejea kazini, na hawa ndio watumishi ambao vile vile walishughulikia huduma za afya wakati Ghaza ilipokuwa inashambuliwa na mabomu; na katika siku mbili ziliopita pekee tumeshahudumia afya wakazi 11,000 katika Ghaza.”