Vijana kusongesha Agenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu - Monicah Malith
Vijana kusongesha Agenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu - Monicah Malith
Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF, kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs limefikia tamati wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wawakilishi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamebadilishana uzoefu kwa takriban wiki mbili kuhusu jinsi ya kusongesha malengo hayo endelevu. Vijana nao hawakuachwa nyuma.
Miongoni mwao ni Monicah Malith kutoka Kenya ingawa asili yake ni Sudan Kusini ambako alipakimbia akiwa na umri wa miaka 12 na sasa ni mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Monicah anaeleza anazoziona ni changamoto za vijana kutoshiriki kikamilifu katika kuyafanikisha malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika kipengele cha mada kwa kina.