Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustadi na jitihada za sungura viwe chachu tunapokabili magumu ya dunia, asema Guterres katika salamu za mwaka mpya wa kichina

Ujumbe wa Katibu Mkuu kwa njia ya video katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina ambao alama yake mwaka huu ni sungura
UN

Masuala ya UM

Chun Jie Kuai Le! Heri ya mwaka mpya wa kichina. Ndio ilivyoanza video ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye ametuma salamu za heri ya mwaka mpya kwa wachina wote ulimwenguni ambao mwaka huu alama yake ni sungura!

Hii leo wachina wanaazimisha mwaka mpya wa kichina, ambao mwaka huu 2023 ni mwaka wa Sungura

Katika video hiyo ya sekunde 45 Guterres amesema “Sungura ni ishara ya bidii na ustadi. Hizo ni sifa tunazohitaji wakati huu ubinadamu ukikabiliwa na magumu na mitihani. “

Ameishukuru China kwa ushirikiano wao mkubwa na Umoja wa Mataifa na ushirikiano wanaotoa kimataifa.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema “Kwa kufanya kazi pamoja kama jumuiya ya kimataifa, tunaweza kuendeleza amani, maendeleo endelevu na ulimwengu bora kwa wote.”

Amehitimisha salamu zake kwa kusema wakati huu ambapo wana matumaini na mwanzo mpya, anawatakia wao na familia zao afya njema, ustawi, na furaha katika Mwaka Mpya wa kichina.