Guterres akutana na rais wa China mjini Beijing.

2 Septemba 2018

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya mazungumzo na rais wa China Xi Jingping leo mjini Beijing na kujadili masuala mbali mbali.

Guterres yuko ziarani China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa ushirikiano baina ya China na Afrika utakaoanza kesho. Jukwaa hilo la ushirikiano kati ya Mataifa 53 ya Afrika na China lilianzishwa mwaka 2000 baada ya mkutano wa mawaziri uliofanyika mjini Beijing 

Mada kuu ya mkutano wa Beijing wa mwaka huu wa 2018 utakaomalizika tarehe 4 September ni ushirika wa ushindi kwa pande zote , kufanya kazi pamoja kwa ustawi wa maendeleo kwa China na Afrika ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

 

UN China/Zhao Yun
Katibu Mkuu Antonio Guterres -katikatikuliaakutana na rais Xijiping wa China katikati kushoto, kabla ya mkutano wa ushirika kati ya China na Afrika mjini Beijing.

Mbali ya viongozi mbalimbali wa mataifa na serikali za Afrika kuhudhuria mkutano huo akiwemo pia mwenyekiti wa tume ya Muungan o wa Afrika , mashirika 27 ya kimataifa na ya kanda ya Afrika yatashiriki.  

Leo jioni, baada ya kukutana na rais Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametembelea makavazi ya Sanaa ya Beijing na bustani ya Beihai. 

Bw Guterres aliandamana na Liu Zhenmin, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na masuala ya kiuchumi na ya kijamii pamoja na balozi Ma Zhaoxu Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter