Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heri ya mwaka wa Simba Marara kwa wananchi wa China: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akitoa ujumbe wa mwaka mpya wa Kichina
UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akitoa ujumbe wa mwaka mpya wa Kichina

Heri ya mwaka wa Simba Marara kwa wananchi wa China: Guterres

Utamaduni na Elimu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatumia ujumbe wa heri ya mwaka mpya wakichina wananchi wa China ambao wanasherekea mwaka wa Simba Marara

Katika ujumbe wake kwa njia ya video Katibu Mkuu Guterres amesema Simba Marara humaanisha ujasiri, nguvu na thabiti na hizo ni sifa zinazohitajika wakati dunia inakabiliana na changamoto za kipekee isizo na kifani za siku hizi.

Naishukuru China na wananchi wake kwa kujizatiti katika ushirikiano wa kimataifa na kwa Umoja wa Mataifa. Nategemea kuendelea kwa usaidizi wenu na ushirikiano katika kusongesha Ajenda Yetu ya Pamoja na kufanikisha matarajio yetu ya pamoja ya kuwa na mustakabali wenye amani na endelevu.Amesema Gutteres

Amebainisha kuwa ili kufanya hivyo, kilamtu anapaswa kuchukua hatua thabiti kushughulikia masuala halisia yanayokabili dunia hivi sasa kama vile mabadiliko ya tabianchi na janga la COVID-19. "Kwa pamoja ni lazima tukwamuke pamoja na tujijenge upya kwa ubora zaidi."

Katibu Mkuu huyo pia amewaarifu wananchi wa China kuwa hivi karibuni anatarajia kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing nchini China. 

“Olimpiki inaangazia kama nguzo ya mshikamano wa binadamu na natarajia kuwa michezo hiyo itakuwa salama na yenye mafanikio.”