Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi Kyangwali Uganda na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali mjini Hoima nchini Uganda
UN/ John Kibego
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali mjini Hoima nchini Uganda

Wakimbizi Kyangwali Uganda na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Nchini Uganda, wakimbizi katika makazi yao ya Kyangwali mjini Hoima, wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa maandamano, shughuli za kitamaduni huku vyote vikimulika umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika juhudi za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi sambamba na  athari za mabadiliko hayo kwao hasa wakimbizi nchini Uganda.  

 

Maandamano yaliongozwa na bendi kutoka Maratatu B hadi Maratatu A katika makazi ya wakimbizi ya kyangwali. Wanajeshi na askari polisi wameshiriki pamoja na vikundi vya wakimbizi kutoka nchi mbalimbali.
Mgeni wa rasmi amekyuwa ni Kamanda wa polisi wa wilaya ya Kikuube, ASP Richard Asiimwe.

Harakati hii iliondaliwa na shirika la Care International Uganda linatekelezwa chini ya kauli mbinu ya siku ya leo ya wanawake duniani, Usawa wa kijinsia leo kwa ajili ya kesho endelevu na kuongeza kutambua umuhimu wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Uganda.

Santa Lamunu ni afisa wa masaual ya ukatili wa kijinsia kwneye shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR Hoima, na akachagiza ulinzi wa wakimbizi dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali mjini Hoima nchini Uganda
UN/ John Kibego
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali mjini Hoima nchini Uganda

Kila baada ya hotuba moja, nyimbo na densi ya kitamaduni vilikuwa vikitamalaki vikibeba jumbe za kukemea ukatili wa kijinsia na uchafuzi wa mazingira.

Kundi la wanawake la Nyakatehe katika jamii jirani ya kambi hii ya wakimbizi ya Kyangwali nalo lilipata fursa ya kutumbuiza.

Unajisi wa wasichana na ubakanji wa wanawake wakati wa kusaka kuni vichakani mbali na nyumbani na kutokuwa na uhakika wa chakula ni miongoni mw amasuala yanayohusisha mabadiliko ya tabiannchi na wanawake.

Noreen Nampewo, ni afisa wa ukatili wa kijinsia na ulinzi wa wakimbizi katika shirika la Care Internaitonal Uganda akasisitiza umuhimu wa ulinzi wa wakimbizi na kubainisha kuwa umuhimu wa mchango wa wanawake katika suala zima la maendeleo endelevu.

Kamanda wa polisi wa wialya ya Kikuube ASP Asiimwe ameelezea uhusiano kati ya wanausalama na masuala ya mendeleo akisema vyote hivyo vinakwenda pamoja huku akiwahakishia wakimbizi kuwapatia ulinzi kwa kukabiliana na wote wanaokiuka haki za binadamu.