Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

  WHO yahaha kukidhi mahitaji ya afya kwa Wapalestina 200,000

Mtoto wa kipalestina akiwa mbele ya bandari ya Gaza ambayo imeharibiwa wakati wa mapigano ya hivi karibuni.
© UNICEF/Eyad El Baba
Mtoto wa kipalestina akiwa mbele ya bandari ya Gaza ambayo imeharibiwa wakati wa mapigano ya hivi karibuni.

  WHO yahaha kukidhi mahitaji ya afya kwa Wapalestina 200,000

Afya

Wakati makubaliano ya usitishaji uhasama katika eneo linalokaliwa la Wapalestina yanaendelea kutekelezwa, shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaongeza juhudi zake za kutoa msaada wa afya kwa karibu watu 200,000 wanaohitaji haraka msaada huo katika eneo hilo. 

Mpaka sasa WHO imetoa dawa muhimu kusaidia huduma za majeruhi na huduma ya gari la kubeba wagonjwa kwa watu zaidi ya 2,000 waliojeruhiwa vibaya katika Ukanda wa Gaza, imetoa mahema kumi yatakayotumiwa na WHO kwa ajili ya matibabu na yamewekwa nje ya idara sita za dharura za katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Dkt. Rik Peeperkorn mkuu wa ofisi ya WHO katika eneo linalokaliwa la Wapalestina (oPt) “Hali ni tete. WHO inaendelea kuwa na wasiwasi juu ya hali hiyo katika OPt na inatoa wito wa kupatikana bila kizuizi kwa huduma muhimu na zinazohusiana na maendeleo na wafanyikazi huko Gaza na kupeleka wagonjwa nje kutoka Gaza kila inapohitajika”.

Na kwa kuwa janga la COVID-19 likiwa bado ni tishio linaloendelea, WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kupitia mkakati wa kimataifa wa chanjo COVAX, wameunga mkono kupelekwa kwa dozi zaidi ya 260,000 za chanjo dhidi ya COVID-19 kwa eneo linalokaliwa na Palestina pamoja zikiwemo dozi 60,000 zilizowasilim leo kutoka kwa WHO na shirika hilo pia linatoa dawa muhimu na vifaa kwa Jerusalem Mashariki. 

Kuanzia tarehe 31 Mei 2021, kumekuwa na wagonjwa 332,191wa COVID-19 waliothibitishwa za vifo 3,765 vilivyoripotiwa katika OPT, na huku idadi ya idadi ya wagonjwa ikiongezeka huko Gaza katika wiki za hivi karibuni.

Mapema vita vya silaha katika eneo linalokaliwa la Palestina vilisababisha kufurushwa kwa watu zaidi na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu wa muda mrefu. 

Uhasama umesababisha kupoteza maisha ya Wapalestina 278 na zaidi ya majeruhi 9,000. Watu wengine zaidi ya 77,000 wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani na karibu vituo 30 vya afya vimeharibiwa, karibu vituo vingine vya afya vya rufaa 600 vimeathiriwa kwa sababu ya kufungwa kwa vivuko wakati wa kuongezeka kwa uhasama.

 Mnamo Mei 20 mwaka huu, WHO ilizindua ombi la dfola za Kimarekani milioni 7 kusaidia shughuli zake za kiafya kwa miezi sita ijayo, likilenga wale waliokumbwa na kiwewe na huduma ya dharura, afya ya akili na huduma za kisaikolojia, uelimishaji na kudumisha huduma muhimu za kiafya ikiwemo huduma za COVID-19. 

Hadi sasa, dola milioni 2.3 zimepokelewa kutoka ombi la dola milioni 7.0 zinazohitajika kwa kipindi cha miezi 6 ijayo.

“Maisha ya Wapalestina yanazidi kudorora, watu wengi walioathiriwa na mzozo wanahitaji msaada wa haraka na wanakabiliwa na vitisho vingine vya kiafya kama COVID-19. WHO inafanya kazi kusaidia mfumo wa afya wa Wapalestina na washirika wake katika kukabiliana na hali ya dharura ya kibinadamu na inatoa wito wa msaada kwa jumuiya ya kimataifa katika juhudi hizi ”, amesema Dkt. Rik Peeperkorn .