Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Watoto katika shule nchini Haiti wakipata chakula kama sehemu ya mpango wa mlo shuleni wa WFP.
UN Photo/Leonora Baumann

Theluthi 2 ya mwaka wa masomo duniani imepotea sababu ya COVID-19:UNESCO

Ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19, Zaidi ya wanafunzi milioni 800 ambao ni zaidi ya nusu ya wanafunzi wote duniani bado wanakabiliwa changamoto kubwa ya kuvurugwa kwa elimu yao, kuanzia kufungwa kwa shule katika nchi 31 hadi kupunguzwa au kusoma kwa muda mfupi katika nchi zingine 48 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo kupitia ramani ya ufuatiliaji ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na utamaduni UNESCO.