Theluthi 2 ya mwaka wa masomo duniani imepotea sababu ya COVID-19:UNESCO

Watoto katika shule nchini Haiti wakipata chakula kama sehemu ya mpango wa mlo shuleni wa WFP.
UN Photo/Leonora Baumann
Watoto katika shule nchini Haiti wakipata chakula kama sehemu ya mpango wa mlo shuleni wa WFP.

Theluthi 2 ya mwaka wa masomo duniani imepotea sababu ya COVID-19:UNESCO

Utamaduni na Elimu

Ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19, Zaidi ya wanafunzi milioni 800 ambao ni zaidi ya nusu ya wanafunzi wote duniani bado wanakabiliwa changamoto kubwa ya kuvurugwa kwa elimu yao, kuanzia kufungwa kwa shule katika nchi 31 hadi kupunguzwa au kusoma kwa muda mfupi katika nchi zingine 48 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo kupitia ramani ya ufuatiliaji ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na utamaduni UNESCO.

Takwimu hizo ambazo zimechapishwa leo siku ya kimataifa ya elimu katika ramani hiyo zinaonyesha kwamba , duniani kote shule zilifungwa kabisa kwa wastani wa miezi 3.5 sawa na wiki 14 tangu kuzuka kwa janga la COVID-19.

Katika maeneo mengine takwimu zimeongezeka hadi miezi 5.5 sawa na wiki 22 ambazo ni theluthi mbili yam waka mzima wa masomo ukizingatia muda wa kawaida wa shule kufungwa.

Kijana barubaru akitumia teknolojia ya maadishi hadi sauti katika shule ya elimu kwa watu wanaoishi na ulemavu Kuala Lumpur, Malaysia.
UNICEF/Pirozzi
Kijana barubaru akitumia teknolojia ya maadishi hadi sauti katika shule ya elimu kwa watu wanaoishi na ulemavu Kuala Lumpur, Malaysia.

Tofauti baina ya kanda na kanda

Kwa mujibu wa twimu hizo za UNESCO kumekuwa na tiofauti kubwa za muda wa ufungaji shule baina ya kanda kuanzia miezi 5 (wiki 20) za wastani wa kufungwa shule kabisa nchi nzima Amerika ya Kusini na nchi za Caribbea hadi miezi 2.5 (Wiki 10) kwa nchi za Ulaya na mwezi mmoja tu kwa Ocenia.

Tofauti hiyo imedhihiria pia wakati wa kuangalia muda wa kawaida wa ufungaji shule ambao unaanzia wastani wa miezi 7 (wiki 29) kwa nchi za Amerika ya Kusini na Caribbea ikilinganishwa na wastani wa miezi 5.5 (wiki 22) kwa maeneo mengine duniani.

Hata hivyo tawimu hizo za ramani ya ufuatiliaji ya UNESCO zinaonyesha kuwa serikali zimejitahidi kupunguza ufungaji shule nchi nzima kutoka nchi 190 wakati wa kilele cha maambukizi ya COVIDF-19 mwezi Aprili 2020 na kufikia nchi 30 leo hii ambapo nchi nyingi zinaunga mkono kufunga sehemu tu ya masomo au kufunga kutokana na maeneo athirika zaidi katika kiala nchi.

Hivi sasa shule zimefunguliwa kikamilifu katika nchi 101 duniani.

Mwanafunzi wa kike nchini Ghana akinawa mikono kwa sabuni kabla ya kurejea darasani ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha elimu inaendelea huku wakidhibiti maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
UNICEF/Geoffrey Buta
Mwanafunzi wa kike nchini Ghana akinawa mikono kwa sabuni kabla ya kurejea darasani ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha elimu inaendelea huku wakidhibiti maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.

Ufungaji shule muda mrefu una athari kubwa

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay akizungumzia suala la kufunga shule amesema“Ufungaji shule wa muda mrefu na wa kujirudia unasababisha ongezeko la athari za kisaikolojia na kijamii kwa wanafunzi, unaongheza kupotea kwa muda wa kujifunza na hatari ya Watoto kuacha shule, na unaathiri kwa kiasi kikubwa jamii zisizpojiweza na zilizo hatarini zaidi. Hivyo ufungaji wa shule kabisa ni lazima uwe suluhu ya miwsho na kufungua shule hizo kwa usalama ndio kiwe kipaumbele.”

Twakimu hizo ambazo zimeandaliwa na kutolewa kitengo cha UNESCO cha ripoti ya kimataifa ya ufuatiliaji wa elimu zinaonyesha kwamba hata kabla ya janga la COVID-19 ni nchi 1 tu kati ya 5 ndio iliyoonyesha hatua kubwa katika usawa wa elimu kupitia mikakati ya ufadhili na kuna ushahidi kidogo sana wa kuwepo usawa katika mikakati ya kukabiliana na COVID-19.

Angures Buba, mwenye umri wa miaka 14 akitafuta masafa ya matangazo ya elimu ya darasa la 8 kwa njia ya redio. Hapa ni kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na masomo anayosubiria kwa hamu ni Sayansi na Kiingereza.
© UNICEF/Helene Sandbu Ryeng
Angures Buba, mwenye umri wa miaka 14 akitafuta masafa ya matangazo ya elimu ya darasa la 8 kwa njia ya redio. Hapa ni kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na masomo anayosubiria kwa hamu ni Sayansi na Kiingereza.

Hivyo Bi. Azoulay amesema“Tunahitaji mkakati uliofadhiliwa wa kujikwamua ili kuweza kufungua shule kwa usalama, tukiwalenga wenye mahitaji zaidi na kuirejesha elimu katika mstari unaotakiwa kwa kizazi cha COVID-19. Leo katika siku ya kimataifa ya elimu natoa wito kwa nchi na washirika wetu kutoa kipaumbele kwa elimu , kwa faida ya dunia nzima katika kujikwamua na janga hili.”

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa janga la COVID-19 litaongeza pengo la ufadhili wa elimu kwa theluthi moja na kugfikia dola bilioni 200 kwa mwaka katika nchi za kipato cha chini na cha kati ambalo ni saw ana asilimia 40 ya gharama zote za elimu.

Na ili kuwezesha s]wanafunzi kurejea salama mashuleni UNESCO imetoa wito kwa walimu na waelimishaji milioni 100 kote duniani kupewa kipaumbele katika kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19.