Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Dola milioni 675 zahitajika ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona:WHO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus, leo Jumatano ametoa ombi la dola milioni $675 million ili kupiga jeki  hatua za kimataifa za kukabiliana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona wakati idadi ya vifo kutokana na homa hiyo ikikaribia 500.