Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 23 baada ya tukio la ugaidi Kenya bado athari zipo-Oscar Ikinya

Oscar Ikinya manusura wa shambulio la bomu la mwaka 1998 nchini Kenya ambapo alipata majeruhi ikiwemo kichwani ambako alama zimesalia miaka 23 baadaye.
Oscar Ikinya

Masuala ya UM

Wakati dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya kumbukumbu na kuwaenzi waathirika wa ugaidi Agosti 21 Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kuendelea kushikamana na waathirika kwani Maisha yao yanabadilika kwa kiasi kikubwa kufuatia matukio waliyoyapitia, Hali ni kama hiyo kwa mgeni wetu wa leo manusura wa shambulio la kigaidi la Kenya la mwaka 1998. Amezungumza na Grace Kaneiya akiwa Nairobi Kenya kwa njia ya mtandao. Katika mazungumzo safari imeanzia miaka 23 iliyopita wakati wa tukio hadi sasa. Karibu.