Msikate miti hovyo kwa kuwa jangwa lanyemelea
Ukataji holela wa miti kinyume na vibali ambavyo vinatolewa na serikali ni moja ya sababu za uharibifu wa mazingira nchini Kenya, amesema Isabella Masinde mtaalam wa mazingira, kutoka idara ya mazingira nchini humo.
Katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Bi.Masinde,Mkurugenzi wa Mazingira na ulinzi wa masuala ya kijamii katika kamati ya kitaifa ya kupokea malalamiko kuhusu mazingira nchini Kenya amesema.miongoni mwa mengine kuwa maendeleo yanaathiri mazingira wakati ..mambo ya kufanya mipango ya matumizi ya hayo mazingira hayatekelezwi, lakini kama kungekuwa na utaratibu wa kujua kama kwa mfano miti ikitolewa miti elfu moja tutaendelea vizuri.