Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Methali ya ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno sasa ni dhahiri huko Kenya

Chebet Lesan, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bright Green Renewable Energy, shirika linalohusika na kutengeneza makaa  yatokanayo na maganda ya vyakula nchini  Kenya, akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN jijini New York, Marekani.

Mkaa wetu hautoi moshi na unaweza ukauwasha, ukauzima na ukauwasha tena.

UN News/Assumpta Massoi
Chebet Lesan, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bright Green Renewable Energy, shirika linalohusika na kutengeneza makaa yatokanayo na maganda ya vyakula nchini Kenya, akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN jijini New York, Marekani.

Methali ya ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno sasa ni dhahiri huko Kenya

Tabianchi na mazingira

Mkaa, mkaa, mkaa tena mkaa utokanao na miti unatajwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa sababu watu wanakata miti na hivyo kuharibu misitu. Misitu ni muhimu siyo tu katika kuweka bayonuai inayohitajika na lishe kwa binadamu, Wanyama na mimea, bali pia hufyonza hewa ya ukaa ambayo inazidi kuongeza ukubwa wa tundu la ozoni kwenye anga kuu.