Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulemavu sio kulemaa tunachotaka ni kujumuishwa: Mbunge Mollel

Amina Mollel, mbunge kutoka Tanzania akiwakilisha watu wenye ulemavu.
UN News
Amina Mollel, mbunge kutoka Tanzania akiwakilisha watu wenye ulemavu.

Ulemavu sio kulemaa tunachotaka ni kujumuishwa: Mbunge Mollel

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Watu wenye ulemavu wanastahili kujumuishwa na kushirikishwa katika mchakato wa ajenda ya maendeleo endelevu SDG's ili ifikapo mwaka 2030 wasisalie nyuma umesema Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu.

Siku hii ya kimataifa ya watu wenye ulemavu inapoadhimishwa kote duniani watu wenye ulemavu wamekuwa wakipaza sauti zao kila kona kwamba ulemavu sio kulemaa wanachohitaji ni ujumuishwashi na miundombinu Rafiki itakayowawezesha kushiriki katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu kama wengine.

Miongoni mwa watu hao ni mbunge Amina Mollel kutoka nchini Tanzania,  yeye mwenyewe ni mlemavu na anawakilisha watu wenye ulemavu wa taifa hilo bungeni, akizungumza nami kwa njia ya simu kutoka mjini Arusha amesisitiza nafasi ya wenye ulemavu katika ujumbe wake