Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiswahili ni lugha ya taifa na kila mtoto ikiwemo walio na ulemavu wafundishwe-Seneta Inimah

Seneta Dkt. Getrude Inimah kutoka Kenya akizunugmza na UN News kuhusu haki za watu wanoishi na ulemavu nchini Kenya

Kutomfunza mtoto lugha yake ta taifa eti tu kwa kuwa ni mwenye ulemavu huo ni unyanyapaa utakaokwamisha mustakhbali wao. Seneta Dkt. Getrude Inimah.

UN News/Assumpta Massoi
Seneta Dkt. Getrude Inimah kutoka Kenya akizunugmza na UN News kuhusu haki za watu wanoishi na ulemavu nchini Kenya

Kiswahili ni lugha ya taifa na kila mtoto ikiwemo walio na ulemavu wafundishwe-Seneta Inimah

Haki za binadamu

Kuwa mlemavu sio kulemaa na unastahili kupata haki zote kama wengine , iwe elimu, afya na hata kutoachwa nyuma katika malengo ya maendeleo endelevu au SDG's, amesema seneta wa Kenya ambaye yeye mwenyewe ni mtu mwenye ulemavu.

Wakati nchi zikiendelea kuweka mikakati katika kuhakikisha zinafikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, bado utekelezaji wa ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma unasuasua katika baadhi ya maeneo. Mathalani kila mtu kuwa mjuzi wa lugha yake ya taifa, bado kuna kasoro. Je ni kwa vipi? Katika makala hii basi  Grace Kaneiya amezungumza na Dkt. Getrude Inimah Seneta katika bunge la Kenya ambaye aliwahi kushuhudia watu walio na ulemavu wa kutosikia wakitengwa mafunzo ya lugha ya kiswahili jambo ambalo ametaja kama unyanyapaa ambao utakwamisha watoto hao katika siku za usoni. Dkt. Inimah ambaye ana ulemavu wa viungo anaanza kwa kuzungumzia namna alivyopokea uteuzi katika bunge, huu ukiwa ni muhula wake wa kwanza bungeni.