Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majaji wanawake Kenya tumeletea mabadiliko chanya - Jaji Okwengu

Jaji Hannah Okwengu wa Mahakama ya Rufaa nchini Kenya

Majaji wanawake huvaa kofia zaidi ya moja; mama, mke na ya jaji na hivyo anakuwa na mtazamo tofauti akikumbuka pia uzoefu wa alikotoka.

Jaji Hannah Okwengu , Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Kenya

Mahakama ya Kenya
Jaji Hannah Okwengu wa Mahakama ya Rufaa nchini Kenya

Majaji wanawake Kenya tumeletea mabadiliko chanya - Jaji Okwengu

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Tarehe 10 mwezi Machi mwaka 2022, kumefanyika maadhimisho ya kwanza ya siku ya majaji wanawake duniani. Siku hii imeadhimishwa na maudhui yakiwa "Haki katika Mtazamo wa Kijinsia." Lengo ni kuona ni kwa vipi majaji wanawake wanaweza kuwa chachu katika utoaji wa haki kwenye mahakama kwa kuzingatia kuwa tasnia hiyo imegubikwa na mfumo dume. Katika kufahamu ukweli wa hoja hiyo Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Jaji Hannah Okwengu wa Mahakama ya Rufaa nchini Kenya ambaye anaanza kwa kuelezea anajisikiaje kuwa Jaji kwenye tasnia iliyozoeleka kuwa ya wanaume wengi zaidi.