25 Agosti 2018

Tume ya sheria ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa mwaka huu wa 2018 imetimiza  miaka 70 tangu iasisiwe. Tume hii Imefanya mengi katika kusongesha masuala ya kisheria. 

Tume ya sheria ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa mwaka huu wa 2018 imetimiza  miaka 70 tangu iasisiwe. Tume hii Imefanya mengi katika kusongesha masuala ya kisheria. Wajumbe wake ambao huchaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wanatoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania. Mjumbe huyo kutoka Tanzania ni Profesa Chris Maina Peter, Mhadhiri  wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam .Yeye akiwa  mjumbe wa tume hiyo hivi karibuni alihudhuria kikao mjini New York, Marekani na katika mahojiano maalum ma Siraj Kalyango wa Idhaa hii ameelezea mengi yaliyotekelezwa na tume ,lakini kwanza anaanza kwa  kueleza mafanikio ya tume hiyo hadi sasa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter