8 Februari 2018

Nchini Tanzania harakati za shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA zimesaidia kuepusha wanawake na watoto wa kike siyo tu dhidi ya mila hatarishi ya ukeketaji au FGM, bali pia zimesaidia kubadili mtazamo wa wanaume kuhusu kuoa wanawake ambao hawajakeketwa. Ali Haji Hamad, afisa wa jinsia kwenye ofisi hiyo amezungumza na Assumpta Massoi kwa idhaa hii.

Maswali ambayo yameulizwa.

  1. Hali ya ukeketaji nchini Tanzania hivi sasa iko vipi?
  2. Nini hasa kichocheo cha mafanikio hayo?
  3. Maghariba imekuwa ni vigumu sana kuachia zana zao kwa kuwa ni mbinu ya kujipatia kipato. Nini kimefanyika?
  4. Bila kukeketwa wasichana wanaona aibu kuolewa na wavulana wanaona aibu kuoa mwanamke hajakeketwa. Nini kimefanyika kubadili mtazamo?

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Maandamano dhidi ya ukeketaji Tanzania. Picha: UNFPA / Mandela Gregoire

Utokomezaji FGM Tanzania sasa watia moyo

Kuelekea siku ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na watoto wa Kike duniani, FGM hapo kesho, nchini Tanzania imeelezwa kuwa kitendo hicho haramu kimepungua na hivyo kutia matumaini. Assumpta Massoi ana taarifa zaidi.