02 APRILI 2024
Pakua
- Leo maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wa misaada 7 wa shirika lisilo la kiselikali au NGO la World Central Kitchen yaliyofanywa na jeshi la Israel, maafisa hao wakirejea kueleza hofu yao kwamba hakuna mahali palipo salia kuwa salama Gaza.
- Tume ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya UNJHRO imesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC.
- Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimishana kuhusu usonji maudhui yakiwa kutoka kuishi kuelekea kwenye ustawi, kwa watu wenye usonji au kwa kiingereza Autism, ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, usonji hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani.
- Na mashinani tunaelekea Gaza kuona ni kwa jinsi gani mashambulizi ya Israel ya hivi majuzi yameathiri huduma za afya katika hospitali ya Al-Shifa.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'38"