Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 MACHI 2024

19 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa mkutano wa leo tunazungumza na Nasra Kibukila ambaye kwa ufadhili wa Mfuko wa Malala (Malala Fund), amewakilisha Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MeT). Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kama zifuatazo. 

  1. Mashirika Umoja wa Mataifa yanayotoa msaada wa kibinadamu huko Gaza hii leo yamesisitiza azma yao ya kusaidia wakazi wa eneo hilo ambako watoto walio hatarini kufa kutokana na njaa kali iliyosababishwa na miezi mitano ya mashambulizi ya Israel na kushindwa kufikishiwa misaada inazidi kuongezeka.
  2. Mwaka 2023 ulikuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika rekodi zote zilizowahi kunukuliwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO katika ripoti yake iliyotolewa hii leo huko Geneva, Uswisi, rekodi za viwango vya joto ardhini, baharini zikivunjwa, barafu na theluji ncha ya kusini zaidi mwa dunia navyo vikiyeyuka. 
  3. Na ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaonesha kitendo cha sekta binafsi kutumikisha watu huzalishafaida isiyo halali yad ola bilioni 236 kwa mwaka ikiwa ni ongezeko la asilimia 37 tangu mwaka 2014.
  4. Katika mashinani tutaelekea katika ukanda wa Gaza ambapo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, katika mwezi mmoja utapiamlo uliokithiri umeongezeka maradufu kaskazini mwa ukanda huo..

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'59"