Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 MACHI 2024

15 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa amani DRC, MONUSCO, na yaliyojiri katika mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?

  1. Hii leo huko jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 10 cha Tanzania (TANZBATT-10) kilichoko kwenye brigedi ya mapigano (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO imekabidhi majukumu kwa kikosi cha 11, TANZBATT-11, katika hafla iliyofanyika eneo la Beni-Mavivi. Msimulizi wetu ni Kapteni Abubakari Muna, Afisa Habari wa TANZBATT-10.
  2. Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa umeingia siku yake ya 5 leo, Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Leo ni baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala. 
  3. Katika makala ambapo hivi majuzi kuliadhimishwa Siku ya Majaji Wanawake Duniani ambayo Umoja wa Mataifa umeendelea kuiadhimisha kila mwaka tarehe 10 Mwezi wa Machi kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa wa kijinsia na kushughulikia masuala ya uadilifu wa mahakama yanayohusiana na jinsia na tunakupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa Hakimu Pamela Achieng.
  4. Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa mtoto mwenye  umri wa miaka 15 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akisimulia jinsi alivyotekwa na makundi yaliyojihami ya waasi lakini hatimaye sasa amenasuliwa na amerejea kwenye jamii kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'5"