Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 JANUARI 2024

17 JANUARI 2024

Pakua

Jaridani leo tunamulika jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis, na suala la kilimo endelevu. Makala tnakuletea mbinu tatu zinazotumika kuhakikisha watoto na familia zao wanapata chanjo na mashinani tutabisha hodi mkoani Mbeya nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu ujuzi unaohitajika ili kufundisha wanafunzi kwa ufanisi.

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehutubia jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis akigusia changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa kuanzia vita inayoendelea Gaza na kwingineko, hali ya kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ya akili mnemba au AI. 
  2. Kilimo kinaweza kuchukua jukumu kuu katika hatua dhidi ya tabianchi wakati huo huo kikihakikisha uhakika wa chakula duniani, ni maoni ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Bayonuai na Mazingira katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Kaveh Zahedi kufuatia hivi majuzi mwaka 2023 kuthibitishwa kuwa mwaka wa joto zaidi katika rekodi za dunia.
  3. Makala hii leo Leah Mushi kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF anatujuza mbinu tatu zinazotumika kuhakikisha watoto na familia zao wanapata chanjo.  
  4. Na katika mashinani Mwalimu Upendo Mwakapala kutoka Shule ya Msingi ya Uhuru iliyoko mkoani Mbeya Tanzania anatujuza mbinu bunifu za kufundisha ili kusaidia kuboresha elimu kwa watoto kupitia Mpango wa Mafunzo ya Ualimu wa Shule za Msingi unaofanikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF na wadau wake.   

Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

Audio Credit
Evarist Mapesa
Audio Duration
10'14"