Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 OKTOBA 2023

02 OKTOBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya makazi, na simulizi ya wakimbizi wa Armania kutoka Karabakh. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni

  1. Mipango ya jamii kudhibiti taka katika maeneo yao inaunga mkono uundaji wa mzunguko wa uchumi, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya leo ya Kimataifa ya Makazi na anaongeza kuwa “juhudi za umma za kupanua maeneo safi ya kijani yanasaidia kupoza maeneo ya mijini nyakati za mawimbi ya joto.”
  2. Nchini Armenia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linahaha kusaidia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo kutoka eneo la Karabakh linalogombewa kati ya Armenia na Azerbaijan ambako sasa idadi ya wakimbizi waliowasili katika kipindi kisichozidi wiki moja ni zaidi ya laki moja na wako taabani.
  3. Makala makala inatupeleka Kenya ambako Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Nairobi Kenya UNIS amezungumza na mmoja wa wazee wastaafu wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho maalum yaliyofanyika leo kuadhimisha siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba Mosi.
  4. Katika mashinani Benedicto Kapaya, mfanyakazi wa kujitolea kutoka Tanzania ambaye ameitikia wito wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO wa kuhamasisha wenyeji wa vijiji vya Muzee na Kalakala kuhakikisha watoto wote wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni ya chanjo inayoendelea nchini humo.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'23"