Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 JUNI 2023

23 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia umuhimu wa watumishi wa umma na walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Afrika Kusinin, kulikoni?

  1. Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wao ni muhimu sana katika ufanikishaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhakikisha mustakbali bora kwa wote. 
  2. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) na wenzao kutoka kikosi cha polisi kinachotoka Senegal wote wakihudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamuhuri wa Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa wiki nzima wamefanya mazoezi ya pamoja ya ulinzi wa amani na kutuliza ghasia hususani wakati nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi wa ngazi mbalimbali ikiwemo kura ya maoni kuhusu katiba. 
  3. Katika makala wiki hii tarehe 21 Juni ulimwengu umeadhimisha Siku ya Yoga Duniani na leo tupo nchini Kenya kumsikiliza Zepline Ouma ambaye kwa miaka mitano sasa anafundisha watu kuhusu mazoezi ya Yoga ambayo uhusisha mtu kutuliza mwili sehemu moja au wakati mwingine kunyoosha viungo na kutafakari kwa utulivu.
  4. Na leo katika mashinani tuankuletea ujumbe wa Nomzamo Mbatha, Mwigizaji na Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini Afrika Kusini ambaye kwake, mamilioni ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao barani Afrika ni kiini cha moyo wake.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
10'41"