Chuja:

Ualbino

UN News/Grece Kaneiya

Tunasherehekea watu wenye ualbino leo kwa sababu tumeona ujasiri wenu na bidii-Muluka Anne

Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Umoja wa Mataifa umetoa  rai kwa nchi zote duniani kuwajumuisha watu wenye ualbino katika mijadala na mipango inayoathiri haki zao za kibinadamu, ili kuhakikisha wanafurahia usawa na ulinzi unaotolewa kwao katika sheria na viwango vya kimataifa.

Sauti
2'24"

13 Juni 2022

Jaridani Jumatatu, Juni 13-2022 na Leah Mushi

-Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa nchi zote duniani kuwajumuisha watu wenye ualbino katika mijadala na mipango inayoathiri haki zao za kibinadamu, ili kuhakikisha wanafurahia usawa na ulinzi unaotolewa kwao katika sheria na viwango vya kimataifa.

Sauti
12'24"
WFP

Kuwatenga wanafunzi wenye ualbino katika shule za peke yao kutaongeza tatizo badala ya kulipunguza-Gamariel Mboya

Umoja wa Mataifa unalenga kupitia malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika kufikia mstakabali bora duniani bila kujali rangi, jinsia au muonekano. Kutoachwa nyuma kunalenga katika mawanda mapana iwe elimu, afya, ajira, haki na wajibu kwa mwanadamu. Katika maeneo mengi duniani, kama ilivyo Tanzania, watu wenye ualbino wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyapaa na hata miundombinu isiyo rafiki kama ya kupata elimu. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, juhudi za kubadilisha hali hiyo zimekuwa zikifanyika.

Sauti
4'3"
UN News/Video capture

COVID-19 imeongeza ugumu katika changamoto za awali za watu wenye ualbino lakini na mwanga upo

Katika kipindi cha takribani miaka kumi nyuma kufikia mwaka 2015 nchini Tanzania kulisheheni matukio mengi ya kutisha yaliyohusisha mauaji au kujeruhiwa kwa kukatwa viungo watu wenye ualbino kutokana na imani za kishirikina. Wadau wa masuala ya haki za watu wenye ualbino wanasema kama si mlipuko wa COVID-19 kuwaongezea matatizo katika changamoto za muda wote kama vile uoni hafifu na matatizo ya ngozi, watu wenye ualbino walikuwa wameanza kuuona unafuu wa maisha kutokana na kupungua kwa matukio ya mauaji dhidi yao.

Sauti
4'12"

12 JUNI 2020

Kuelekea siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino kesho tarehe 13 mwezi Juni, baadhi ya watanzania wenye ualbino wamepaza sauti ya kile wanachoomba kifanyike kuwanusuru wakati huu wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Wamepaza sauti hizo huko Dodoma, mji mkuu wa Tanzania wakati wakihojiwa na Devotha Songorwa wa Radio washirika Kids Time FM.

Na katika kujifunza Kiswahili, Neno la wiki-MANUVA linachambuliwa na Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA, Onni Sigalla.

Sauti
9'53"
UNICEF/Frank Dejongh

Wanafunzi wenye ualbino tuna mahitaji mengi ili kuboresha taaluma yetu

Kama ilivyo nia ya jumla ya Malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa yaani SDGs kuwa asiwepo hata mmoja atakayeachwa nyuma katika kufikia maisha bora duniani, wanafunzi wenye ualbino katika shule ya msingi Mazinyungu iliyopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro Tanzania, wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia mahitaji muhimu kama vile mafuta ya kupaka, nguo za kufunika sehemu kubwa ya mwili wao, Kofia na miwani ili kuongeza ufaulu mzuri hasa kwa wenye uoni hafifu.

Sauti
3'22"
UN News/Video capture

Licha ya kupungua kwa mashambulio dhidi ya watu wenye ualbino, wanaishi kwa mashaka na hofu

Ingawa vitendo vya watu wenye nia ya uovu wa kuwashambulia watu wenye ualbino kuonekana kupungua, bado watu wenye ualbino wanaishi kwa mashaka na hofu kutokana na madhila wanayopitia katika maisha yao ya kila siku.

Kwa mtoto Mwigulu Matonange Magesa mwenye umri wa miaka 16 kutoka Tanzania kwa sasa, vitendo hivyo vimemsababishia kupoteza mkono wake mmoja katika kisa hiki anachosimulia alipohojiwa na Priscilla Lecomte kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya watu wenye Ulemavu uliofanyika mjini New York Marekani. Ambatana nao katika makala ifuatayo.

Sauti
5'30"