Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 FEBRUARI 2023

22 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea habari kuhusu mwelekeo wa matumizi ya maji barani Afrika, na elimu kwa watoto waliotumikishwa jeshini nchini DR Congo.  Makala tutakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunarudi tena nchini DR Congo.

  1. Ni wakati kufikiria upya jinsi ya kutumia maji kwa njia endelevu na yenye uwiano huku ubunifu katika kilimo ukiwa kitovu cha mipango yote, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limesema Qu Dongyu hii leo wakati akizungumza na viongozi na wataalamu wa Afrika kwenye warsha ya kwanza ya kikanda kuhusu mwelekeo wa matumizi ya maji barani Afrika, warsha inayofanyika nchini Zimbabwe.
  2. Mradi mpya wa shule nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC uliozinduliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF na wadau wake kwa ufadhili kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza elimu kwenye maeneo ya mizozo, Education Cannot Wait, ECW, au Elimu Haiwezi Kusubiri umewezesha watoto waliokuwa wametumikishwa vitani kuanza kurejea kwenye masomo na hata kutangamana na wenzao kwa amani.
  3. Katika makala tunakupeleka Njombe mkoa ulioko kusini mwa Tanzania kusikia harakati za Umoja wa Mataifa na wadau za kusongesha ulaji wa mazao ya jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.
  4. Na katika mashinani tutaelekea tena Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumsikia mvulana aliyekuwa ametumikishwa vitani.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'41"