Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

mnepo

FAO

Jamii Somaliland zasaidiwa kupambana na uhaba wa chakula: FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linaendesha mradi wa miaka minne wa mnepo wa uhakika wa upatikanaji wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na migogoro pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi katika pembe ya Afrika lengo likiwa ni kujenga amani na kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo.

Video ya FAO ikimuonesha Asha Mohammed Ali mama wa watoto 8 na mkulima kutoka wilaya ya Wadaamago huko Somaliland akiwa shambani anapalilia mazao yake huku akisimulia namna ukame ulivyowaathiri wakulima na kuharibu kabisa mustakabali wa maisha yao.

Sauti
1'45"
Photo: UNWTO

UN: Kujenga mnepo katika sekta ya utalii ni muhimu ili kuhimili majanga kama COVID-19

Leo ni siku ya mnepo katika sekta ya utalii duniani, na Umoja wa Mataifa unahimiza umuhimu wa kujenga mnepo katika sekta hiyo kwa kuwa ni chanzo cha kipato na ajira kwa mamilioni ya watu lakini pia kuweza kuhimili mishtuko na majanga makubwa kama COVID-19.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa nchi nyingi zikiwemo zenye maendeleo duni, mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea, nchi za Afrika na nchi za kipato cha kati “utalii ni chanzo kikuu cha uchumi, pato la nje, kodi na ajira.” 

Sauti
2'48"

11 JANUARI 2023

Jaridan hii leo tutakupeleka nchini Uganda na Somalia. Makala tutamulika uanzishaji wa vikundi vya vijiji vya kukopa na kuweka akiba na kuimarisha ujuzi wa kidigitali na kifedha, na mashinani nchini tunakwenda nchini Ghana, kulikoni?

Sauti
12'35"

Tuondoe vikwazo vya kitamaduni na kimazingira dhidi ya watu wenye ulemavu- Guterres

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu, Umoja wa Mataifa unapigia chepuo marekebisho yatakayoondoa vikwazo dhidi ya kundi hilo ili malengo ya maendeleo endelevu yanufaishe watu wote.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake amesema msingi mkuu wa kufanikisha hilo ni kuweka mazingira ambamo kwayo hakuna mtu atakayeona ametengwa au ameenguliwa katika kufanikisha malengo hayo.

Mathalani amesema kuwepo kwa miundombinu, teknolojia, huduma na bidhaa ambazo zitanufaisha watu wote wakiwemo watu bilioni moja wenye ulemavu duniani.