Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Somaliland

Wakimbizi wanendelea kuwasili Ethiopia baada ya kukimbia mapigano nchini Somalia.
© UNHCR/Muluken Tadesse

Ukata ni changamoto ya kuwasaidia wakimbizi wa Somalia walioko Ethiopia: UNHCR

Ethiopia inakabiliwa na dharura nyingi huku kukiwa na changamoto kubwa ya  ufadhili duni limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kuongeza kuwa huku kukiwa na watu wapya na wanaoendelea kutawanywa  na kuteseka kutokana na ukame, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inahaha kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya watu waliokimbia makazi yao nchini kote.

08 MACHI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya wanawake duniani, na kilimo Somaliland nchini Ethiopia.  Makala tutatatasalia hapa Makao Makuu na mashinani na tutasikia ujumbe wa kutoka kwa FAO kwa ajili ya wanawake hususan wa vijijini kwa siku hii ya wanawake duniani.

Sauti
12'16"
FAO

Jamii Somaliland zasaidiwa kupambana na uhaba wa chakula: FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linaendesha mradi wa miaka minne wa mnepo wa uhakika wa upatikanaji wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na migogoro pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi katika pembe ya Afrika lengo likiwa ni kujenga amani na kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo.

Video ya FAO ikimuonesha Asha Mohammed Ali mama wa watoto 8 na mkulima kutoka wilaya ya Wadaamago huko Somaliland akiwa shambani anapalilia mazao yake huku akisimulia namna ukame ulivyowaathiri wakulima na kuharibu kabisa mustakabali wa maisha yao.

Sauti
1'45"
Geti la kuingia kwenye makao makuu ya ofisi ya haki za binadamu OHCHR mjini Geneva Uswis
UN Photo/Jean-Marc Ferré

Uchunguzi huru na wa haki lazima ufanyike dhidi ya waliokufa Laas Canood: Turk

Kutoka Geneva nchini Uswisi Kamisha Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Volker Turk ametoa wito kwa mamlaka ya Somalia kuhakikisha uchunguzi huru unafanyika bila upendeleo kufuatia mauaji yaliyotokea baada ya mapigano makali kuanzia tarehe 5 mwezi huu wa Februari nchini humo kati ya vikosi vya usalama na wanajamii wa ukoo wa Laas Canood.

11 JANUARI 2023

Jaridan hii leo tutakupeleka nchini Uganda na Somalia. Makala tutamulika uanzishaji wa vikundi vya vijiji vya kukopa na kuweka akiba na kuimarisha ujuzi wa kidigitali na kifedha, na mashinani nchini tunakwenda nchini Ghana, kulikoni?

Sauti
12'35"