Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 DESEMBA 2022

23 DESEMBA 2022

Pakua

Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 23 ya mwezi Desemba mwaka 2022 tnakuletea habari za WHO na habari kuhusu machafuko jimboni Upper Nile nchini Sudan kusini.  Makala tunakwenda nchini CAR na mashinani nchini Kenya.

  1. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema mwaka 2022 umegubikwa na changamoto lukuki za kiafya , kuanzia janga la COVID-19, Ebola, Mpoxy hadi vita vilivyokatili na kujeruhi wengi hata hivypo linasema kuna matumaini kwa mwaka ujao, yapi?
  2. Nchini Sudan Kusini mapigano ya kikabila kwenye jimbo la Upper Nile nchini humo yamesababisha vifo, ukimbizi wa ndani halikadhalika madhila zaidi kwa watoto ambao mustakabali wao unazidi kuwa mashakani huku nao wazee wakishuhudia machungu katika taifa hilo changa zaidi duniani.
  3. Makala tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR katika mji wa Berberat ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha sita yaani TANZBATT 06 wamekabidhi mradi wa madarasa kwa ajili ya chuo cha kufundishia elimu ya TEHAMA kupitia kopyuta.
  4. Na tutaelekea katika kambi ya wakimbizi Kalobeyei nchini Kenya ambako tutasikia umuhimu wa kuwa na wanawake viongozi.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'14"