Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Lisbon

Kadir van Lohuizen/NOOR/UNEP

Jamii zilizo jirani na bahari ni wadau wakuu katika kulinda bahari- Soares

Baada ya siku tano za mijadala na maonesho mbalimbali, mkutano wa pili kuhusu baharí umefikia tamati huko Lisbon nchini Ureno ambako Miguel de Serpa Soares ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisheria amesema mwelekeo wa kulinda na kuhifadhi baharí unatia matumaini kwa kuzingatia yaliyokubaliwa, changamoto zilizoko sambamba na fursa. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Sauti
1'54"

28 Juni 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiendelea mjini Lisbon, Ureno kujadili suluhu za kukabiliana na changamoto za bahari tunakuleta mada kwa kina ikimulika eneo la Vanga Kilifi huko Kenya wanachi wamepata moja ya suluhu kubwa ambayo ni kuvuna na kuuza hewa ukaa kutoka kwenye mikoko kupitia mradi wa Vanga Blue Forest VBF, ambao kwa kiasi fulani unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP. 

Sauti
11'40"
UN News/Devotha Songorwa

Mabadiliko ya sera kuhusu bahari ni muhimu

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu bahari unaendelea huko Lisbon, Ureno. Mkutano huu umeanza tarehe 27 mwezi huu wa Juni na utamalizika tarehe 1 Julai 2022. Kabla ya kuanza kwa kikao cha ngazi ya juu, mkutano ulitanguliwa na jukwaa la vijana likileta pamoja wanaharakati na wachechemuzi vijana kuhusu masuala ya baharí wakionesha ubunifu wao wa jinsi ya kutatua dharura ya baharí, kama alivyooiita Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres .Miongoni mwa washiriki ni kijana Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dare es salaam nchini Tanzania.

Sauti
1'32"