Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

KILIFI

03 OKTOBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na inatupeleka Kibokoni, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya ambako mabwawa ya samaki yamebadili kabisa maisha ya wavuvi wa eneo hilo walioathirika na mabadiliko ya tabianchi yaliyosabisha samaki kutoweka baharini na kuwakatisha tamaa ya Maisha. Lakini sasa kupitia mradi wa ufugaji samaki ulio chini ya mwamvuli wa Umoja Self-Help Group jamii hiyo ina mabwawa 17 ya samaki yanayozalisha samaki aina ya milkfish, kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na perege au tilapia. Mshiani tanakuletea ujumbe kusu afya ya uzazi na uswa wa kijinsia. 

Sauti
11'35"
UNICEF Kenya

Makala: Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya

Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ukifanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine,lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya  ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.

Sauti
4'13"
Agnes Juma na watoto wake wawili, yeye ni mama wa watoto watano kutoka Kilifi Kenya,  ambaye ni mnufaika wa mradi wa NICHE.
UNICEF Kenya

Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya: UNICEF

Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF unafanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine, lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya  ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.

Sauti
4'13"

12 JULAI 2022

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anafungua jarida:

Habari kwa Ufupi zikimulika wito matumizi ya chanjo zilizoko na kasi katika uzalishaji wake, kisha suala la umuhmu wa mawasiliano ya kimkakati kwenye operesheni za ulinzi wa amani ili kudhibiti taarifa za uongo na potofu, pamoja na kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongeza muda wa azimio la usafirishaji wa shehena kwenda Syria kupitia mpaka wa taifa hilo na Uturuki.

Sauti
9'58"

28 Juni 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiendelea mjini Lisbon, Ureno kujadili suluhu za kukabiliana na changamoto za bahari tunakuleta mada kwa kina ikimulika eneo la Vanga Kilifi huko Kenya wanachi wamepata moja ya suluhu kubwa ambayo ni kuvuna na kuuza hewa ukaa kutoka kwenye mikoko kupitia mradi wa Vanga Blue Forest VBF, ambao kwa kiasi fulani unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP. 

Sauti
11'40"