Asante FAO kwani sasa nimeweza kujipatia zaidi ya dola Elfu 3 kupitia kilimo cha kisasa
Wanawake wa vijijini wanatambuliwa kimataifa kupitia siku yao ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 mwezi Oktoba. Mwaka huu maadhimisho yamefanyika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania, huko Afrika Mashariki. Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula, FAO liliandaa tukio maalum la kutambua mchango wa wanawake hao hasa kwa kuzingatia mchango wao katika uzalishaji chakula, kwani shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO linasema wanawake ni zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi kwenye sekta ya kilimo.