Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 Agosti 2020

12 Agosti 2020

Pakua
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
-   Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya vijana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito kwa viongozi na watu wazima kote duniani kufanya kila linalowezekana kuwawezesha vijana wa ulimwengu kufurahia maisha ya usalama, utu pia fursa na kuchangia katika hatua za pamoja za kimataifa.   
 - Nchini Lebanon, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamezindua kampeni iitwayo Umoja wa Matafa kwa ajili ya Beirut, au UN4Beirut kwa lengo la kuonesha mshikamano na kusaidia watu wa Lebanon kusafisha mitaa ya mji huo mkuu uliosambaratishwa na mlipuko mkubwa wa tarehe 4 mwezi huu wa Agosti.
- Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milišić amesema kitendo cha taifa hilo la Afrika Mashariki kutotegemea misaada ya kigeni ni miongoni mwa sababu zilizowezesha kuingia katika uchumi wa kati. 

- Na kwenye makala  ikiwa leo ni siku ya vijana tutakwendaa nchini kenya katika siku ya kimataifa ya vijana kumulika ubunifu wao katika kupambana na janga la kimataifa la corona.

- Na leo mashinani tutakwenda nchini Uganda kusikia jinsi wanafunzi wanavyotumia muda wao wakati huu ambapo shule zimefungwa na jinsi UNICEF inawasaidia Karibu!

 

 

 

 

 

 

 

 
 
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'24"