UN Tanzania yampongeza msichana aliyeandika mashairi ya SDGs
Kuweka ujumbe wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs katika mashairi ni moja ya njia nzuri za kuyaleta karibu malengo hayo karibu na watu, kuyaelewa na kuyafanyia kazi. Hayo ni maneno ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Millisic alipokuwa akipokea kitabu cha mashairi 17 ya SDGs kilichoandikwa na kijana mtanzania, Aisha Kingu.