Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

8 Aprili 2020

8 Aprili 2020

Pakua

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)

ASSUMPTA:Ni Jumatano 08 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI

1: Afrika imejiandaa kukabiliana na COVID-19 lakini yahitaji msaada:Dkt. Moet 
Wakati janga la mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kuitikisa dunia na kusababisha athari kubwa ikiwemo kupoteza maisha ya maelfu ya watu bara la Afrika mabalo japo halina wagonjwa wengi linahitaji msaada ili kudhibiti kusambaa kwa virusi hiyo.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moet akizungumza na Umoja wa Mataifa nakuongeza kwamba pamoja na changamoto zinazolikabili bara hilo  ambalo sasa limefikisha wagonjwa  zaidi 10,000 wa COVID-19, nchi zinajitahidi kufanya ziwezalo
(SAUTI YA DKT.MOET CUT 1)
“Ninatiwa moyo sana na hatua ambazo zimepigwa kwa ujumla na nchi hadi sasa, lakini pia kuhusu uwezo wa upimaji kwa sababu ndio kitovu cha nini wanachotakiwa kufanya , mwezi mmoja na nusu uliopita kulikuwa na maabara mbili tu katika nchi mbili ambazo upimaji ulikuwepo lakini sasa nchi 41 katika kanda ya Afrika zinaweza kupima virusi hivi , hii ni hatua nzuri. “
Ameongeza kuwa nchi za Afrika zimepiga hatua pia katika uchunguzi kwenye maeneo ya kuingia na kutoka ikiwemo viwanja vya ndege na mipakani na pia baadhi ya viongozi na wakuu wa nchi wametambua umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti kudhibiti kuenea kwa mlipuko huo ikiwemo marufuku ya mikusanyiko, kutotembea hovyo , watu kusalia majumbani , kufunga mipaka na kuhakikisha usafi wa kunawa mikono kwa sabuni akitolea mfano Kenya, Afrika kusini na Rwanda.
Hata hivyo Dkt. Moet amesema pamoja na jitihada zinazofanyika bara hilo linahitaji msaada ili kupiga hatua katika baadhi ya maeneo
(SAUTI YA Dkt.MOET CUT 2)
“Maeneo ambayo bado yanahitaji kupigwa hatua yanajumuisha kuhakikisha kwamba tuna vitu na vifaa katika nchi vya kwanza kuwalinda wahudumu wa afya , vifaa vya kujikinga, kuvipata vifaa hivi, na vifaa vya kupimia maabara ni muhimu sana. Tunakiri kwamba baadhi ya vitu hivi viko nje ya uwezo wa serikali, kimataifa pia kuna changamoto ya soko na baadhi ya vitu hivi ni vigumu kupatikana. Pia kuna haja ya kuimarisha ufuatiliaji kwa kina na uzoefu wetu katika kutoa huduma ni haba tutahitaji kutumia uwezo tulionao kwa njia bora zaidi.”
===================================================

2: Ujuzi tulioupata wakati wa Ebola tutautumia kupambana na COVID-19-Wauguzi DRC
 
Wakati mlipuko wa ugonjwa Ebola ukielekea kufikia ukingoni nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, wahudumu wa afya waliopata mafunzo wakati wa janga hilo, hivi sasa wanatumia ujuzi walioupata, kuimarisha mfumo wa afya nchini humo ikiwa  ni pamoja na kutumia uwezo huo kupambana na virusi vya corona, COVID-19 Grace Kaneiya na maelezo zaidi.
 
(Taarifa ya Grace Kaneiya)
 
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema kama hakuna mgonjwa yeyote mpya atakayetokea, mlipuko wa sasa wa Ebola nchini DRC utatangazwa kufikia ukomo katikati ya mwezi huu wa Aprili, 2020. 
 
Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini DRC walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na Ebola. Walipokea mafunzo na vifaa kutoka WHO na washirika wake ili kuwasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola, huku wakijilinda wao wenyewe kutoambukizwa.
 
Muuguzi Esperance Kavira Kavota ni mmoja wa wauguzi ambaye kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu amefanya kazi katika kituo cha kutoa tiba ya Ebola katika mji wa Beni, moja ya vitovu vya mlipuko wa Ebola. Na sasa kwa kuwa mlipuko wa Ebola unaelekea mwisho, amerejea kazini katika wodi ya wanawake wanaojifungua katika Hospitali ya Beni. Katova anaeleza uzoefu kama wenye kuleta msongo mwanzoni kutokana na kukutana kwao na wagonjwa ambao wameambukizwa.
 
(Sauti ya Kavota)
 
“Hatukuwa na vitu vya kujikinga, tulikuwa tunavaa tu aproni za mpira, glovu na barakoa. Hivyo tu. Kisha muungano wa kimataifa wa hatua za tiba (ALIMA), na WHO wakaja. Mashirika yote waliweka nguvu yao pamoja na sasa tunafahamu jinsi ya kujitenga vizuri na kituo hiki cha Ebola kikajengwa.”
 
Uzoefu walioupata wahudumu hawa wa afya, pamoja na miundombinu ya Ebola iliyojengwa inaweza kutumika kuimarisha mfumo wa afya na kupambana na milipuko mingine kama Ebola. Bi Kavota anaendelea
 
(Sauti ya Kavota)
 
“Kabla ya mlipuko huu wa Ebola, hatukuwa na mafunzo ya kuzuia na kudhibiti maambukizi au mafunzo  kwa ajili ya kushughulikia waliofariki au hata ufahamu kuhusu tiba mahususi ya Ebola. Lakini baadaye tulipokea mafunzo kuhusu virusi vya Ebola na tiba yake. Wageni wengi walikuja hapa na uzoefu wao na wakatufundisha. Walitupatia vifaa ambavyo hatukuwa tumevitumia kabla, na mbinu nyingi mpya. Zilitusaidia. Katika tukio la mlipuko mwingine, tutaweza kuushughulikia kwa wakati unaofaa.”
 
Kavota anasema wakati huu ambao Ebola inaelekea ukingoni, wauguzi kama yeye watakuwepo wakati wote kuhudumia hospitali kwa uwezo wao wote. 

====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: Na punde ni makala ambapotunasikia sehemu ya pili ya makala kuhusu madhila anayekumbana nayo mwanamke kipofu vitani na hata ukimbizini.
====================================================

3: Mradi wa UNDP Tanzania wabadili maisha ya wakazi wa Bunda mkoani Mara
Nchini Tanzania mradi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha nyanya unaofadhiliwa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, katika wilaya ya Bunda mkoani Mara umebadili maisha ya wakazi wa eneo hilo na hivyo kufanikisha lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, la kutokomeza umaskini. Taarifa zaidi na  Flora Nducha.
(Taarifa ya Flora Nducha)
Nats..
Wilaya ya Bunda mkoani Mara tupo katika shamba la kikundi cha wakulima cha Bulamba.
Wakulima hawa wengi wao awali walikuwa wanashughulika na uvuvi lakini sasa wanapata stadi za kilimo cha kisasa cham boga na wanapokea maelekezo kutoka kwa Afisa kilimo Elad Didas Tarimo, hapa  wakitaka kufahamu kuhusu wadudu waharibifu wa nyanya..
Nats…
Ni kutokana na mafunzo hayo kupitia chama cha wakulima wa mboga na matunda Tanzania, TAHA, nyanya zimestawi vizuri na sasa ni heka heka za mavuno,  wanawake,  wanaume na vijana na ndoo zao za nyanya. Hamasa ni kubwa na mchelewaji shambani  hakosi kauli kutoka kwa wenzake…
Nats..
Mkulima huyu ni Tabu Paulo, almaarufu Mama Rock City ni mnufaika wa mradi huu wa mwaka mmoja ambaye anasema.
(Sauti ya Tabu Paulo)
Nimeanza kulima nyanya tarehe 1 mwezi Novemba mwaka 2019. Na kilimo hiki Miongoni mwa changamoto ilikuwa  mvua hapa na pale lakini hizo zote tumezihimili. Nyanya yangu iko sokoni kwa sasa, inang’aa na haina madoa na inavutia. Kwa wanawake wenzangu nawaomba waache kubweteka nyumbani, waje waangalie kilimo tulichofanya hapa kupitia UNDP. Kwa hiyo naomba hii nyanya tukiiuza kwa mauzo tutakayopata kwa mvuno huu wa kwanza tuweze kulima shamba jingine kwa kutumia kilimo cha kisasa zaidi yaani iwe mara mbili ya hapa. Kwa hiyo naomba tuletewe teknolojia zingine mpya za mazao mengine ya bustani ili tuweze kuendeleza mazao mengine mbalimbali ili na sisi tuweze kuajiri watu wengine ili wapitie kwenye mikono ya UNDP na TAHA.
Mradi wa aina hii unaolenga vijana na wanawake unatekelezwa pia katika wilaya za  Same, Arumeru na Busega na UNDP inapanga kupanua zaidi iwapo fedha zitapatikana.

 
===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA: 
Na sasa ni makala mapisha John Kibego anayezungmuza na mzee Donata Nyirakaboozi mkimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyeko latika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali.
=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
====================================================

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:

Shukrani John Kibego kwa makala hiyo
====================================================
Na sasa ni  mashinani ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dokta Tedros Ghebreyesus anazungumzia mwongozo mpya wa kuvaa barakoa katika kukabiliana na janga la virusi vya ugonjwa wa Corona, au COVID-19.
 ===================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA:
Shukrani sana Dokta Tedros Ghebreyesus
==================================================
STUDIO: Play Bridge

ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Tupatane kesho kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York.

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'13"