Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 Machi 2020

23 Machi 2020

Pakua

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)      

ASSUMPTA:Ni jumatatu  ya  Machi Ishirini na tatu mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI 

1: Uganda yafunga mipaka yake kwa abiria juu ya COVOD-19
                                
Serikali ya Uganda imeamua kufunga mipaka yake yote kwa abiria na kutangaza kuwa ni vyombo vyenye shehena za mizigo pekee ndio vitakavyovuka mipaka na kuingia nchini humo kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona au  COVID-19 nchini humo mwishoni mwa wiki. Maelezo zaidi na mwandishi wetu, John Kibego kutoka Kampala.
(Taarifa ya John Kibego)
Hatua hii imetangazwa katika hotuba ya Rasisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa taifa baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya Corona aina ya COVID-19 kuthibitishwa humo ncjhini.
Kisa hicho kilithibitishwa usiku wa kuamkia tarehe 22 mwezi huu wa Machi na kutangazwa na Waziri wa Afya Dokta Jane Ruth Aceng kwenye mkutano wa wandishi wa habari.
Kisa hicho cha COVID-19 ni cha raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 36 naliyekuwa amerejea nyumbani kutoka safari yake ya kibiashara mjini Dubai.
Kufuatia kisa hicho, huyu hapa Riais Museveni akibana usafiri wa aabiria, kuingia au kutoka ndani ya nchi.
(Sauti ya Museveni)
“Kutokana na utata wa kujaribu kudhibiti wasafiri kutoka nchi zilizoathiriwa sana, tuliamua kusitisha kabisa usafiri wa abiria kuingia au kutoka ndani ya Uganda. Ni bora tuokoe nyumbani ambayo ni Uganda na watu milioni 42 waliomo. Naam tunafahamu kuwa kuna Waganda nje ya nchi lakini kama tulivyokuwa tikufanya vitani ikiwa kambi imevamiwa, tunatoa kipaumbele kwa kushinda wavamizi wa kambi. Ndio maana tumesema hamna abiria tena iwe kwa ndege, nchi kavu au usafiri wa majini. Pia tumesema kwamba hatutakubali watu kuingia hata kwa basikeli au wanaotembea kwa mguu kupitia kwenye mipaka rasmi au isio rasmi kwani tutapeleka askari huko”
Kilithibitishwa saa chache baada ya ibaada maalum iliyofanyika kwneye ikulu ya Raisi ya Entebbe na kuhudhuriwa na karibu vyongozi wa dini zote kwa ajili ya kuliombea taifa lisisajili kisa chochote cha virusi hivyo na pia kumshukuru Mungu kwa kulilinda dhidi ya wmambukizo wakati ambapo nchi nne jirani za Tanzania, Rwanda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zinakumbana na milipuko.
Mlipuko nchini Uganda pia umetangazwa siku tatu baada ya kufungwa kwa taasisi zote za elimu, masoko yanayolema na mikutano ya kisiasa na maeneo yote ya mijumwiko ya umma kama njia ya kuzuia mlipuko.
Magari, ndege na boti za mzigo ndizo zitakubaliwa kufanya kazi ya kuvuka mpaka lakini kwa masharti ya kuzingatia usadi na maagizo yote ya wizara ya afya na pia lazima kila chombo kimoja kisiwe na wafanyakazi wanaozidi watatu.
Raisi Museveni amewashauri wananchi wasitumie tena usafiri wa umma ikiwa wana uwezo wa kutumia usafiri binafsi au kujizuia safari sisizo za dharura.
Kwanzia jioni ya Ijumma, takribani watu 100 wamekamatwa na kuzuiliwa kwenye korokoroni mbalimbali kote nchini kuhusiana na kukaidi maagizo ya Raisi ya kinga dhidi ya COVID-19.

===================================================

2: Wafanyakazi wenye ulemavu CCBRT Tanzania wapatiwa mafunzo ya dhidi ya COVID-19
Nchini Tanzania mafunzo kuhusu virusi vya Corona na jinsi ya kukabiliana navyo ambayo yanatolewa kwa watendaji wenye ulemavu katika hospitali ya CCBRT yemekuwa na manufaa makubwa wakati huu ambapo tayari taifa hilo la Afrika Mashariki limethibitisha kuwa na wagonjwa wa virusi hivyo. Ni kwa vipi basi? Tuungane na Hilda Phoya mwanafunzi anayefanya mafunzo kwa vitendo katika kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam ambaye amevinjari katika hospitali hiyo.
(Taarifa ya Hilda Phoya)
Nimefika katika hospitali ya CCBRT iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam ili kufahamu uelewa wa watendaji wenye ulemavu katika kukabiliana na virusi vya Corona.
Baada ya kutumia viuavisumisho ili kutakatisha mikono yangu nakutana na Abdalla Majule, mfanyakazi  CCBRT ambaye amenieleza..
(Sauti ya Abdalla Majule)
“Nimejifunza vizuri zaidi tofauti na mwanzo nilikuwa naona kwenye vyombo vya habari na kusikia. Leo nimepata kitu kikubwa, kwa sababu tumefundishwa vizuri jinsi gani ya kujikinga. Kama una virusi vya Corona ni vyema wewe ukavaa barakoa kuliko yule ambaye hana Corona, vinginevyo wale wanaohudumia wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya Corona wao ndio wanaweza kuvaa barakoa.”
Naye Jestina Mdoe ambaye ni kiziwi akizungumza kupitia mtafsiri wa lugha, Suzan, ameshukuru mafunzo waliyopatiwa ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya Corona lakini amezungumzia suala la kuwapatia viziwa habari akisema.
(Sauti ya Jestina Mdoe)
“Mara nyingine tunapata usiku kwenye televisheni mbalimbali,  na baadhi ya sisi tunaotumia lugha ya alama, lakini wakati mwingine tunapata vikwazo, kwa sababu watu wanaozungumza na wanaosikia wao wanaelewa, lakini sisi viziwi tunatumia lugha ya alama. Ni lazima tuweze kuona na  kama mkalimani yupo kwenye televisheni sauti au picha ni ndogo, kwa hiyo mimi na matatizo ya macho inawezekana kuangalia sielewi na picha yenyewe siwezi kuona na kuielewa vizuri. Kwa hiyo naomba sana kuwasisitiza viziwi waalikwe na lugha ya alama itumike kuwapatiwa mafunzo na Mungu awabariki.”

====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: Na Punde ni mashinani tunaungana na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, Dkt. Tedros Ghebreyesus.Baki nami!
====================================================

3: Kamwe sitakata tamaa. Nitashinda!-Nakout Slylvia
 
Nakout Sylvia alitekwa nyara na kikundi cha waasi cha Uganda mnamo 2003 na alikamatwa mateka kwa miaka 12 huko Afrika ya Kati. Kama matokeo ya unyanyasaji wa kijinsia wa kila mara, aliambukizwa Virusi Vya UKIMWI, VVU. Nakout baadaye alifanikiwa kutoroka na akapata hifadhi nchini Finland ambako sasa ameanza kujifunza mchezo wa gofu wa frisbee ambao ni maarufu nchini Finland. Je maisha yake hivi sasa yako vipi? Grace Kaneiya anasimulia zaidi.

(Taarifa ya Grace Kaneiya)
 
Nats
 
Nafikiri haya ni maisha bora ambayo nimewahi kuwa nayo tangu nimezaliwa.Niko imara, na wakati mwingine najihisi kama siumwi.
 
Ni Nakout mkimbizi kutoka Sudan Kusini anayeishi nchini Finland ameanza kujifunza kucheza fresbee golf, mchezo maarufu wa Gofu nchini Finland, anasema,
 
(Sauti ya Nakout)
 
“Inakufanya uwe  sawa kimwili na mwenye utulivu.Inaua msongo wa mawazo kwa namna unavyozunguka, zunguka. Unaporudi nyumbani, ukaoga maji baridi na kulala, unajisikia kuchoka sana.Ni mazoezi mazuri.”
 
Nakout alitekwa na waasi wa LRA mnamo mwaka 2003 na akateseka kwa miaka kwa manyanyaso ya kingono. Alitoroka na sasa anaishi na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.
 
(Sauti ya Nakout)
 
“Nilikuja Finland katika nyakati ambazo nilikuwa siwezi kulala. Nilikuwa nalala kwa kunywa dawa za usingizi. Hali yangu ya kiafya ilikuwa mbaya. Nilikuwa nazidiwa kila siku. Lakini tangu nilipowasili Finland tarehe 28 mwezi Mei mwaka jana, ninaona mabadiliko mengi.Ninaona bado nina matumaini ya maisha ndani yangu.”
 
Nakout ameanza kujifunza lugha ya kifin inayozungumzwa nchini Finland.Na anawafundisha lugha ya kiingereza wakimbizi wengine na katika video hii ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anaonekana akiwa katika shughuli yake hiyo ya kujifunza na kufundisha.
 
Na baadaye anaahidi kutoshindwa katika njia yake mpya ya kucheza Gofu.
 
(Sauti ya Nakout)
 
“Tulikuwa tunacheza watatu lakini mara zote wananishinda, kwa kuwa bado mimi ni mpya katika mchezo huu. Lakini sitakata tamaa. Ninawaahidi kuwa msimu wa kaingazi ujao, nitawashinda. Sina wasiwasi. Sikati tamaa. Ndiyo, siwezi.Sitakata tamaa hata iweje.”
 

===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  Na sasa ni wasaa wa sehemu ya pili ya makala ambapo Saa Zumo wa Redio washirika Pangani FM amepita katika mitaa ya Pangani mkoani Tanga kusikia maoni ya wananchi kuhusu ugonjwa wa COVID-19 au virusi vya corona..

=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
==================================================== 

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  

Shukrani Saa Zumo kwa makala hii.
====================================================
Na sasa ni  mashinani tuungane na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la  Afya la Umoja wa Mataifa, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus anayeelezea jinsi vijana wanapaswa kukabiliana na virusi vya corona.

====================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA: 
Asante sana Dokta Tedros kwa ujumbe huo.
==================================================
STUDIO: Play Bridge
ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Hadi wakati mwingine kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo ni……na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York. 

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'28"