Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo ya viwanda Afrika yaende sanjari na ajenda 2030: Guterres

Maendeleo ya viwanda Afrika yaende sanjari na ajenda 2030: Guterres

Pakua

Uwekezaji madhubuti katika miundombinu baina ya nchi utasaidia kuboresha biashara na kuinua uwezo wa viwanda barani Afrika.

Hilyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 20.

Ameongeza kuwa kuchagiza teknolojia zinazojali mazingira na kutumia kiwango kidogo cha hewa ukaa vitatoa fursa ya kuongeza biashara na ukuaji wa viwanda.

Amesisitiza kuwa wajasiriamali wadogo na wa wastani ambao tayari wanachangia asilimia 80 ya pato la taifa la bara hilo na kutoa asilimia 90 ya ajira watasailia kuwa wadau wakubwa katika maendeleo ya viwanda barani humo.

Amezitaka serikali , wafanyabiashra na asasi za kiraia kudumisha ushirika ili kuongeza kasi ya ubunifu na kuchagiza ukuaji endelevu. Amesema itakuwa muhinmu sana pia kuhakikisha uwezo wa vijana unapewa fursa katika kuimarisha taasisi barani Afrika kwa ajili ya ajenda ya amendeleo endelevu ya 2030 na ajenda ya Afrika ya 2063.

Amekumbusha kuwa Umoja wa Mataifa utaendele kusaidia maendeleo barani Afrika ili kuwa na bara huru na lenye mafanikio kwa watu wake wote.

Photo Credit
Uwekezaji madhubuti katika miundombinu baina ya nchi utasaidia kuboresha biashara na kuinua uwezo wa viwanda barani Afrika. Picha: UM