Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya polisi ikianza UM, mchango wao ni muhimu kwa operesheni za ulinzi:Carrilho

Wiki ya polisi ikianza UM, mchango wao ni muhimu kwa operesheni za ulinzi:Carrilho

Pakua

Juma hili makamishina wa polisi wa Umoja wa Mataifa kutoka katika sehemu mbalimbali za operesheni za amani za Umoja huo wamekusanyika kwenye makao makuu hapa mjini New York Marekani kuanzia leo ili kuwasilisha ripoti zao kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Mshauri mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya polisi Luis Carrilho ndiye mwenyeji wa makamisha hao na anasema polisi wana mchango mkubwa kwenye operesheni za ulinzi na usalma za moja wa Mataifa na mkutano huu ni muhimu

(CARRILHO CUT 1)

“Wiki ya Umoja wa Mataifa ya polisi ni muda wa kipekee kwa makashimisha wa polisi kutoka kwenye operesheni za ulinzi wa amani na washauri maalumu wa polisi katika operesheni za kisiasa kukutana New York na kubadilishana mawazo na uzoefu na mara watakaporejea katika operesheni zao kuweza kutoa huduma bora kwa jamii na kwenye operesheni walizoko.”

Kama mshauri mpya wa masuala ya polisi wa Umoja wa mataifa kwa miaka miwli ijayo ametaja kipaumbele chake

(CARRILHO CUT 2)

‘Ni kufanya kazi kwa motisha na kujitolea katika maeneo tuliyo na polisi wa Umoja wa mataifa , ili kuhakikisha watu ambao wanaishi katika maeneo yaliyo na polisi wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi kwa pamoja na wenzetu wa ulinzi wa kijeshi na wafanyakazi wa kiraia ili kuweza kutoa huduma bora.”

Photo Credit
Mshauri mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya polisi Luis Carrilho.(Picha:UM/Video Capture)