Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msiwape mgongo waeritrea wanaokimbia ukiukwaji wa haki za binadamu- Bi Keetharuth

Msiwape mgongo waeritrea wanaokimbia ukiukwaji wa haki za binadamu- Bi Keetharuth

Pakua

Raia wa Eritrea wanateseka kutokana na ukiukwakaji wa haki za bindamu na maelfu wanaendelea kutembea kutwa kucha wakisaka hifadhi nchi jirani.

Sheila B. Keetharuth ambaye ni mtaalamu wa haki za binadamu kuhusu Eritrea amesema hayo akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Ameelezea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo na kutolea wito jamii ya kimataifa kuonyesha mshikamano wao na wale wanaohatarisha maisha yao na kuvuka mipaka ambako jeshi linatekeleza amri ya kuua kwa kupiga risasi.

Bi Keetharuth ametaja ukiukwaji kama kukamatwa kiholela na bila fursa ya kuwasiliana na familia au kutoweshwa kwa wale wasiofuata amri kama miongoni mwa madhila yanayowakabili wa Eritrea.

Ameongeza kuwa juhudi za kupunguza idadi ya wakimbizi wanaowasili huenda zikapunguza idadi lakini hakutozuia watu kuvuka majangwa na bahari ili kutafuta usalama kwani hakuna kitu chochote kitakachomzuia mtu anayekimbia ukiukwaji wa haki zake.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, Eritrea haina Katiba ya kulinda haki za msingi, haina mahakama huru, au bunge wala taasisi yoyote inayoweza kulinda raia dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka na taifa.

Photo Credit
Sheila B. Keetharuth, Mratibu Maalum kuhusu haki za binadamu Eritrea. Picha ya UN/Jean Marc Ferré.