Uhakika wa usalama eneo la Wau ni kichocheo cha watu kurejea nyumbani-Shearer

Uhakika wa usalama eneo la Wau ni kichocheo cha watu kurejea nyumbani-Shearer

Pakua

Usalama ndio kitu ambacho wakazi wa Wau, Kaskazini Magharibi mwa Sudan Kusini wanahitaji ili kuweza kurejea nyumbani.

Hiyo ni kauli ya Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer katika mahojiano maalum na radio ya ujumbe wa umoja huo nchini humo UNMISS.

Akizungumza baada ya ziara yake katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Lokoloko, Shearer amesema amezungumza na gavana na mamlaka za kiusalama na kusema kwamba wengi wa wakimbizi wanahofia safari za usiku kurejea nyumbani kwani..

(Sauti ya Shearer)

“Hatuwezi kuhakikishia watu usalama, ni nje ya uwezo wetu, kuna makundi mengi ya watu waliojihami, kuna ukatili unaotekelezwa na watu waliojihami ikiwemo uporaji, unyanyasaji, mauaji na kubaka yote yanafanyika, lakini iwapo hali ya kawaida itarejea na watu waanze kurudi nyumbani basi hiyo itawashawishi wengine kwani watu watapata ujasiri iwapo majirani na marafiki zao watakuwepo.”

Bwana Shearer ambaye pia ni mkuu wa UNMISS ameongeza kwamba ni muhimu usalama urejee lakini pia hakikisho la misaada ya kibinadamu kwa wale wanaorejea Wau ili kuchagiza watu kurudi nyumbani.

Photo Credit
Ukarabati katika kambi eneo la Wau nchini Sudan Kusini.(Picha:UNMISS)