Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusibabaike na kukosolewa kwa UNRWA bali tuiunge mkono:Guterres

Tusibabaike na kukosolewa kwa UNRWA bali tuiunge mkono:Guterres

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anawasiwasi na kukosolewa hadharani kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Palestina, UNRWA na uadilifu wake, lakini anaunga mkono na kupongeza mchango wake katika ulinzi wa haki za mamilioni ya wakimbizi wa Palestina walio Mashariki ya Kati.

Amesema UNRWA inafanya kazi katika hali ngumu ya kivita, ikitoa elimu kwa nusu milioni ya wasichana na wavulana wakimbizi kuhusu haki za binadamu na uvumilivu, elimu na msaada ambao unachangia kwa kina utulivu katika eneo hilo.

UNRWA imepewa mamlaka hiyo na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambalo limekiri mara kwa mara mchango wake mkubwa na wa kipekee katika amani na usalama wa eneo hilo.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa nchi wanachama kuendelea kuunga mkono UNRWA katika kutimiza kwa uadilifu na ufanisi mamlaka yake, pia katika kutumikia wakimbizi wa Palestina hadisuluhu ya muda mrefu itakapopatikana.

Photo Credit
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM / Jean-Marc Ferré