Skip to main content

Janga laibuka polepole huko Idlib, Syria- Pinhero

Janga laibuka polepole huko Idlib, Syria- Pinhero

Pakua

Mkuu wa kamisheni huru ya uchunguzi kuhusu Syria, Paulo Pinheiro, ameonya leo kuhusu janga linaloibuka pole kule Idlib, akisema kamisheni hiyo ina wasiwasi kuwa maisha ya watu wanaohamishiwa huko yamo hatarini.

Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kikao cha faraghani cha Baraza la Usalama, Bwana Pinhero amesema pande zinazozozana aghalabu hutumia mbinu za kijeshi zinazowalenga raia, kama njia ya kujinufaisha kijeshi.

Amesema pande zote zilikiuka haki za binadamu wakati wa na baada ya kuzingirwa mji wa Aleppo, na hivyo kupelekea makubaliano ya kuwahamisha raia yaliyosababisha watu kulihama kabisa eneo la mashariki ya mji.

Photo Credit
Mkuu wa kamisheni huru ya uchunguzi kuhusu Syria, Paulo Pinheiro.(Picha:UNIfeeed/video capture)