Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatikanaji wa tiba dhidi ya kifua kikuu Tanzania

Upatikanaji wa tiba dhidi ya kifua kikuu Tanzania

Pakua

Moja ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza janga la ugonjwa wa kifua kikuu au TB ifikapo mwaka 2030. Mkakati wa shirika la afya ulimwenguni, WHO wa kutokomeza TB unataka kupunguzwa kwa vifo vitokanayvo na ugonjwa huo kwa asilimia 90 na kupunguza visa vyake kwa asilimia 80. Malengo haya yatafikiwa iwapo tiba sahihi itapatikana kwa wakati sahihi kwa wagonjwa, pia mikakati ya kuzuia kueneza ugonjwa. Je nchini Tanzania upatikanaji wa huduma ya TB ukoje? Basi ungana na Kelvin Mpinga wa redio washirika Pangani Fm ya Tanga Tanzania ambaye amezungumza na mratibu wa kifua kikuu na ukoma wilaya ya Pangani Dkt. Erick Msechu, kwanza ameanza kumuuliza takwimu za ugonjwa wilayani humo

Photo Credit
Tiba dhidi ya Kifua Kikuu huhusisha matumizi ya mchanganyiko wa dawa. Picha: UM