Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi bora ya fedha za umma yataimarisha kilimo Afrika

Matumizi bora ya fedha za umma yataimarisha kilimo Afrika

Pakua

Benki ya Dunia imetaka nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zifanyie marekebisho mfumo wake wa matumizi ya fedha za umma ili kupatia kipaumbele sekta ya kilimo.

Katika ripoti yake kuhusu Kuvuna faida zaidi:Vipaumbele vya matumizi ya umma Afrika kwa ajili ya tija kwenye kilimo, benki hiyo imesema kwa sasa bajeti za serikali bado ni finyu na hivyo ni lazima kubadili mwelekeo kwa sekta hiyo iliyo uti wa mgongo kwa ukuaji wa uchumi.

Makamu Rais wa Benki ya Dunia kwa bara la Afrika Makhtar Diopo amesema ili kutokomeza umaskini na kuinua tija barani humo, kilimo lazima kipatiwe kipaumbele.

Kwa mantiki hiyo ripoti inataka marekebisho ili matumizi au sera zozote za kuboresha kilimo kama vile ruzuku, pembejeo na teknolojia vilenge wakulima maskini, kwa kuwa hivi sasa wanufaika ni matajiri.

Photo Credit
Mkulima huyu na miche ya Acacia akiwa kijiji cha Launi, Aguie, Niger.(Picha:IFAD)