Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twampongeza na tutahakikisha usalama wa Jameh

Twampongeza na tutahakikisha usalama wa Jameh

Pakua

Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Uchumi wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Muungano wa Afrika (AU) kwa kauli moja, umepongeza ukarimu na uzalendo wa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jameh baada ya kuamua kuhamisha madaraka kwa Rais Adama Barrow jana jioni.

Katika tamko lao la pamoja,  Umoja wa Mataifa, ECOWAS na AU umeahidi kushirikiana na serikali ya Gambia kuhakikisha rais wa zamani Jameh pamoja na familia yake, wafuasi wake  na wale waliokuwa chini ya uongozi wake watapewa hadhi, heshima na usalama nchini Gambia na hakutakuwa na kitendo cha vitisho na unyanyasaji na utungaji wa sheria dhidi yake au mali yake iliyo halali.

Tamko hilo limesema kuwa rais huyo wa zamani ataondoka nchini humo kwa muda bila ya chuki yoyote ili kusaidia utaratibu mzuri na amani wa uhamisho wa madaraka kwa serikali mpya, na kwamba itahakikisha uwezo wake wa kurejea nchini Gambia wakati wowote atakapoamua bila ya vikwazo vyovyote.

Vile vile imesema itahakikisha usalama katika nchi zitakazoamua kumkaribisha na kumhifadhi.

Pia ECOWAS imeahidi kusimamisha shughuli zote za kijeshi nchini  humo na wote wameahidi kushirikiana na mamlaka ya Gambia katika mchakato wa maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Photo Credit
Watoto wakicheza katika mto nchini Gambia. Picha:OCHA/Ivo Brandau