Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Ukraine wanaendelea kukabiliwa na ukiukwaji wa haki:UM

Raia wa Ukraine wanaendelea kukabiliwa na ukiukwaji wa haki:UM

Pakua

Mgogoro ambao bado haujatatuliwa Ukraine unaendelea kukatili maisha ya raia na kuwaacha wengine maelfu katika hatari kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu , umeonya leo Alhamisi Umoja wa Mataifa.

Katika ripoti mpya kuhusu mgogoro huo ulioanza mwaka 2014, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kwamba jamii zilizo katika msitari wa mbele wa mapigano Mashariki mwa nchi hiyo bado wako katika hatari ya vita, mabomu na vifaa ambavyo havijalipuka.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa pia imeelezea kwa kina madai yanayoendelea ya ukatili namashitaka dhidi ya Tatars kutoka jimbo la Crimea na makundi mengine yaliyopigwa marufuku nchini Urusi.

Ripoti hiyo pia inasema umoja wa mataifa unatiwa hofu kwamba serikali na makundi ya upinzani nchini Ukraine hawafanyi juhudi za kutosha kuwalinda wasio wapiganaji, ikitaja uharibifu mkubwa katika shule, vituo vya afya na vituo vya kulelea watoto.

Photo Credit
UN Photo.